Ijumaa, 19 Aprili 2013

WANANCHI WAISHTAKI SERIKALI KWA CCM MGOGORO WA KIWANDA CHA MTIBWA NA WAKULIMA WA MIWA

1 
Ndugu Andurahman Kinana Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM wakizungumza nawawakilishi wa  wananchi wa Mtibwa Wilayani Mvomero ambao waliishitaki serikali kwa Chama cha Mapinduzi  kutokana na migogoro lukuki inayoawaandama wananchi hao ambao ni wakulima wa miwa na wafugaji, walillamikia uongozi wa kiwanda cha mtibwa kutowalipa vizuri katika mauzo ya miwa ikiwani pamoja na kuchelewesha mafao ya wastaafu na kuchelewesha michango ya wafanyakazi katika mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF. Jambo hilo limoenekana kuwa tatizo sugu kwa viongozi wengi wamepita huko mtibwa na kuambiwa matatizo ya mgogoro huo katika ya kiwanda cha Mtibwa Sugar na wakulima , Katika hatua za kutatua mgogoro huo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana amewaita wawakilishi wa Wakulima wa Miwa wawakilishi wa Wafugaji, wawakilishi wa Harlamashauri ya Wilaya Mvomero Uongozi wa Mtibwa na Mkuu wa Wilaya ya Mtibwa ambao watakutana siku ya Jumatatu Aprili 22 mjini Morogoro na kujadiliana juu ya kumaliza mgogoro huo. Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Honolulu mjini Turiani Mtibwa mkoani Morogoro.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-TURIANI 2 
Wawakilishi hao wakimsikiliza Ndugu Abdurahman Kinana alipokuwa kaizungumzia hatua za kuchukua ili kutatua mgogoro huo 3 
Abdurahman Kinana akizungumza katika mkutano huo kutoka kulia ni Sadik Murad Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM, Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Ndugu Sixtus Mapunda,Katibu wa Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro  INNOCENT KALOGERIS 4 
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Mtibwa Sugar Hamad Yahya akijibu hoja za wananchi mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana 5 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Jonas Vanzeland akizungumza katika mkutano huo ambapo ameutuhumu uongozi wa Mtibwa Sugar kwa kuwakata fedha ya kodi wakulima, fedha ambayo ilitakiwa kulipwa na wao, lakini pia akaongeza kwa wanalimbikiza deni kubwa kiasi kwa limefikia zaidi  milioni 500, kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Anthon Mtaka. 7 
Wananchi wa mtibwa wakinyoosha mikono yao juujuu ili kupata nafasi ya kutoa dukuduku lao mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana. 8 
Abdurahman Kinana akimsikiliza Ismail Hamad Mwenyekiti wa CCM chuo Kikuu cha Mzumbe wakati akimuelezea juu ya kongamano lao ambalo litafanyika kesho mkoani Morogoro likihusisha vijana wa sekondari , vyuo vikuu na vijana wa mtaani katika kuzungumzia dhana nzima ya uzalendo na kuenzi amani iliyopo nchini, wanaomsikiliza ni wanafunzi wenzake wa Mzumbe ambao ni wana CCM. 9 
Ndugu Andurahman Kinana Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM akiwasili kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Mabao mjini Turiani Mtibwa.  12 
Wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano huo 13 
Kikundi cha Makilikili kikitumbuiza kabla ya mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mabao. 14Kutoka kushoto ni Jaquline, Nasrah na Kisa wadau kutoka CCM tawi la Mzumbe 15 
Katibu Mkuu wa CCM akiwahutubia wananchi wa Turiani Mtibwa Wilayani Mvomero 17 
Kulia ni Wadau Okta kulia Edo kushoto na Ndugu Mtanda  Mbunge wa Nchinga. 18 
Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana wakati akiwahutubia leo mjini Turiani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...