Washiriki
wa kongamano la siku mbili la Uhuru wa Habari Duniani wakijiandikisha
kabla ya kuanza rasmi kwa mkutano wa Siku mbili katika kuadhimisha Siku
ya Uhuru wa habari duniani linalofanyika jijini Arusha katika Hoteli ya
Naura Springs.
Mgeni
rasmi katika siku ya Uhuru wa Habari Duniani Katibu mkuu wa Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera akiwasili na kusalimiana na
viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo
katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha kufungua Kongomano la siku
mbili la Uhuru wa habari kwa wahariri na waandishi wa habari na wadau
mbalimbali wa habari
Mwakilishi
wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akisalimiana na
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard
Sezibera mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya Naura Springs jijini
Arusha kufungua Kongamano la siku mbili la wahariri na wanahabari pamoja
na wadau wa habari katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari
ulimwenguni.
Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard
Sezibera (katikati) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magessa
Mulongo (kushoto) pamoja na Katibu Mtendaji wa MOAT Bw. Henry Muhanika
wakiingia ndani ya ukumbi wa mkutano wa Kilimanjaro katika Hoteli ya
Naura Springs jijini Arusha.
MC
katika Kongamano la Uhuru wa Vyombo vya habari ulimwenguni Usia Nkoma
kutoka kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akitambulisha meza
kuu ya wageni katika kongamano hilo.
Meza
Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera (wa pili kulia) na Mwakilishi wa
Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen (wa tatu kushoto).
Picha
juu na chini Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki
Balozi Dr. Richard Sezibera akihutubia na kufungua Kongamano la Siku
Mbili linaloenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari
Duniani.
Na. Mahmoud Ahmad Arusha
Katibu
mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard Sezibera leo
amefungua rasmi kongamano la waandishi wa Habari Tanzania pamoja nchi
wanachama wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika kuadhimisha ya siku
ya uhuru wa Habari Duniani uliobeba kauli mbiu “USALAMA NA MAZINGIRA
BORA YA KUFANYIA KAZI KWA WAANDISHI WA HABARI NA WAARIRI AFRIKA YA
MASHARIKI”
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kaongamano hilo la waandishi wa habari
liliofanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Naura
springs amesema kuwa kongamano hili la vyombo vya Habari pamoja na
wamiliki lina umuhimu kwa sababu litaifanya jamii pamoja na serikali
kujua nini umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika maendeleo ya
nchi na jamii yote.
Amesema
kuwa uhuru wa vyombo vya habari kwa kiasi kikubwa unajikita katika
uhuru wa kutoa maoni na pamoja na uhuru wa kutoa habari hivyo katika
kuelewa hilo vyombo vya habari vinatakiwa viwe vinafanya kazi zake
pasipo kutegemea upande wowote ili kisije kuchochea au kuvunja amani ya
nchi kama ilivyotokea miaka ya nyuma kwa nchini Rwanda na Burundi.
Aidha
amesema kuwa kuna changamoto kubwa sana zinazozikumba vyombo vya habari
hususani vyombo vya kijamii ambapo wanakuwa na mazingira magumu ya
kutafuta habari na kufanya wakati mwingine waandishi kuwa katika
mazingira hatarishi kwa maisha yao pamoja na hali mbaya ya kiuchumi
inayopelekea kutoweza kufanya kazi kuendana na mabadiliko ya sayansi na
Teknolojia ikiwepo kujiingiza katika mawasiliano ya mkongo wa kitaifa.
Kongamano
la mwaka huu limeratibiwa na MISSA TANZANIA kwa kushirikiana na EAJA,
Mfuko wa vyombo vya Habari Tanzania ( TMF), Muungano wa club za
wandishi wa habari (TPC), Umoja wa Mataifa Tawi la Tanzania, Baraza la
Habari Tanzania (MCA), Wamiliki wa Vyombo vya habari Nchini (MOAT) pamoj
na kituo cha habari kwa wananchi TCIB na kudhaminiwa na Shirika la
UNESCO.
Picha juu na chini baadhi ya washiriki wakifuatilia kongamano hilo sanjari na hotuba ya mgeni rasmi.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Magessa Mulongo akitoa salamu za Serikali wakati wa
kongomano la siku mbili katika kuadhimisha siku Uhuru wa habari
lililofanyika leo jijini Arusha.
Mwakilishi
wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akitoa Ujumbe wa
Pamoja wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
Irina Bokovas kuhusiana na Siku ya Uhuru wa Habari Duniani ulioenda
sambamba na Kongamano la Uhuru wa vyombo vya Habari katika nchini za
Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo kwenye Hoteli ya Naura
Springs jijini Arusha.
Picha
juu na chini ni Meza kuu na washiriki wa Kongamano la Uhuru wa Habari
Duniani wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka aliyekuwa mwandishi wa
habari na Mwenyekiti wa Iringa Press Club Marehemu Daudi Mwangosi
aliyeuwawa mkoani Iringa wakati akitimiza majukumu yake ya kazi ya kila
siku.
Mkurugenzi
wa Habari Maelezo Bw. Assah Mwambene (kushoto) akiwa na wadau pamoja na
Balozi wa Sweden nchini Mh. Lennarth HJELMAKER (kulia) aliyeambata na
mkewe katika kongamano hilo.
Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi akiwa na mtoto wa mwisho wa marehemu katika Kongamano hilo.
Pichani
ni mmoja wa washiriki akionyesha bango lililokuwa na tukio la kuuwawa
kwa Mwandishi wa Daudi Mwangosi ambalo limeandikwa” HABARI NI MUHIMU
KATIKA UJENZI WA TAIFA, UKIMUUA MWANDISHI WA HABARI UMEUA DEMOKRASIA,
HAKI NA MAENDELEO YA NCHI YAKO”.
Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard
Sezibera akikabidhi hundi ya Shilingi Milioni 5 kwa Mjane wa Marehemu
Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi iliyotolewa na Umoja wa Vilabu vya
waandishi wa habari Tanzania (UTPC) kumsaidia kuendesha maisha yake.
Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard
Sezibera na Mwenyekiti wa UTPC Tanzania Bw. Abubakari Karsani (kulia)
kwa pamoja wakimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi Milioni 5 Mjane wa
Marehemu Daudi Mwangosi Bi. Itika Mwangosi.
Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Dr. Richard
Sezibera akizungumza na mtoto wa mwisho wa Marehemu Daudi Mwangosi mara
baada ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 5 kwa mjane wa marehemu.
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin kutoka UNESCO akifuatilia mada mbalimbali wakati wa kongamano hilo la Uhuru wa Habari Duniani.
Mama Rahma wa Ofisi za Unesco Tanzania na Usia Nkhoma wa UNIC Dar.
Msanii
wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akitoa ujumbe wa waandishi wa habari
kwenye siku ya Uhuru wa Habari mbele ya mgeni rasmi na viongozi
mbalimbali wa mashirika ya umoja wa mataifa na Serikali.
Mgeni
rasmi akimfungua plasta mdomoni mmoja wa wasanii wa Band ya Mrisho
Mpoto kama ishara ya kuwapa uhuru waandishi wa habari kuzungumza kilio
chao mbele ya mgeni rasmi kama ujumbe wa siku ya Uhuru wa Habari
Duniani.
Wasanii
wa Mrisho Mpoto wakiimba kwa hisia kali kuelezea madhila wayapatayo
waandishi wa habari wawapo kazini ikiwemo usalama wao katika kazi zao za
kila siku.
Mzee Kassim Mapili akiongoza Band ya Mrisho Mpoto kutoa burudani mara baada ya kongamano hilo kufunguliwa.
Mkurugenzi
wa Habari-Maelezo Bw.Assah Mwambene (kushoto) akisalimiana na Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard
Sezibera.
Mgeni rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera akiteta jambo na Balozi
wa Sweden nchini Mh. Lennarth HJELMAKER nje ya ukumbi wa mikutano wa
Kilamanjaro katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
Mgeni
rasmi Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard
Sezibera akiagana na Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania
Vibeke Jensen ambao ndio wafadhili wa Kongamano hilo.
Afisa
Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa
(UNIC) Bi Stella Vuzo (katikati) akiagana na Mgeni rasmi Katibu mkuu wa
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Balozi Dr. Richard Sezibera mara baada
ya kuzindua Kongomano la wahariri wa vyombo vya habari pamoja na
waandishi ikiwa ni mwendelezo wa sherehe za Siku ya kuadhimisha Uhuru wa
vyombo vya habari ulimwenguni.
Maveretans
wa Tasnia ya Habari wakiwa na Mkurugenzi wa Misa Tan Tumaini Mwailege (
wa tatu kushoto) na Wa kwanza Kushoto ni Mama Eda Sanga, Mama Rosemary
Haji wa UNESCO, Leila Shekha na Theophil Makunga wakifurahi baada ya
kukutana katika Kongamano hilo.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wakongwe katika tasnia ya Habari walioshiriki katika Kongamano hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni