Pichani
ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete akiwa na Ndugu Justine Peter Mwandu (kushoto). (Picha na
Maktaba).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Justine Peter Mwandu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Taarifa
iliyotolewa leo, Ijumaa, 03 Mei, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu
Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza
Aprili 28, mwaka huu, 2013.
Kabla ya uteuzi huu, Ndugu Justine Peter Mwandu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu katika Shirika hilo.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
03 Mei, 2013
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni