Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Ndugu. Adam H. Mayingu tuzo ya kuwa Mfuko wa kwanza wa Hifadhi ya Jamii Tanzania kutoa mikopo ya nyumba kwa wanachama wake. Tuzo hiyo ilitolewa kwenye maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Mifuko ya Jamii mjini Dodoma. Mh. Raisi alisema PSPF ni mfuko madhubuti na una fursa nyingi za kimaendeleo kwa wananchi wa Tanzaniai na unauwezo mkubwa na salama katika uwekezaji . Aliongezea kwa kusema sio kweli kwamba Mfuko huu uko mahututi kama ilivyozungumziwa kwenyebaadhi ya vyombo vya habari, bali Mfuko huu unadai wadai wake Trilioni 6 na kudai sio kufilisika tena
Mtangazaji wa TBC Amina Mollel akikabidhi fomu ya kujiunga na PSPF kwa Meneja Masoko wa Mfuko huo Bi. Costantina Martin mala baada ya kuvutiwa na kukata shauri ya kuwa mwanachama wa Mfuko wa kwa njia ya uchangiaji wa hiari
Timu ya PSPF iliyokuwa kwenye maonyesho ya wiki ya hifadhi ya Jamii wakiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wao ndugu Adamu Mayingu katikati. Timu hiyo inastahili pongezi kutokana na uduma bora waliyokuwa wakiitoa kwa wananchi waliokuwa wakitembelea banda hilo la PSPF pale Nyerere squire Dodoma.
Wanachama wa PSPF wakipata taarifa mbalimbali ikiwapo historia ya michango yao na taarifa za uanachama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni