Jumanne, 14 Mei 2013

TWIGA CEMENT YASAIDIA WAHANGA WA MAFURIKO ARUMERU ARUSHA.

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (katikati mwenye suti nyeusi) akipokea sehemu ya msaada wa mifuko 200 ya Cement kutoka kwa Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza, iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Arusha mwishoni mwa wiki.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (katikati mwenye suti nyeusi) akimshukuru  Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza, baada ya kupokea  msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na kampuni hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni.
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (kulia) akizungumza  baada ya kupokea  msaada wa mifuko 200 ya saruji iliyotolewa na kampuni ya Twiga Cement kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni. Kulia kwake ni  Meneja Meneja Mahusiano Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’Souza.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na pia Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Ole Medeye (aliyeshika kamba kulia) akisaidia maandalizi ya ujenzi wa daraja sehemu iliyoharibiwa na mafuriko katika hafla ambayo kampuni ya  Twiga Cement ilikabodhi msaada wa saruji  kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua katika kijiji cha Marurani na maeneo jirani wilayani Arumeru Mkoani Arusha hivi karibuni.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...