Jumatatu, 13 Mei 2013

Ujenzi wa ofisi za matawi ya CCM Singida Mazala achangia shilingi laki tatu taslimu.

Mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala akisalimiana na Wana-CCM wa tawi la Mwaja na wananchi kwa ujumla alipokwenda Mwaja kuweka jiwe la msingi la ofisi ya tawi la CCM.
Mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala akiweka jiwe la msingi katika jengo la ofisi ya CCM tawi la Mwaja kata ya Mandewa.
Mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) taifa manispaa ya Singida, Hassan Mazala akihutubia wanaccm na wananchi wa kijiji cha Mwaja  muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ofisi ya CCM tawi la Mwaja.
Mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) taifa manispaa ya Singida,Hassan Mazala akimkabidhi mwanachama mpya wa CCM Asha Muna (68) kadi ya kujiunga na chama hicho tawala.
Baadhi ya viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ofisi ya CCM tawi la Mwaja.
Baadhi ya wananchi wakazi wa kijiji cha Mwaja waliohudhuria hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ofisi ya CCM katika kijijini humo.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) taifa manispaa ya Singida Hassan Mazala, ameagiza matawi yote ya CCM kuweka mikakati madhubuti ya kujenga ofisi zenye hadhi inayofanana na Chama Cha Mapinduzi.
 Mazala amesema matawi kuwa na ofisi za kisasa, kunasaidia sana kuwavutia wanaccm na wananchi kwa ujumla,kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi-chama tawala.
Mnec huyo ametoa changamoto hiyo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ofisi ya tawi la CCM kijiji cha Mwaja kata ya Mandewa Singida mjini.
 Amesema ujenzi wa ofisi za matawi ni sehemu muhimu katika kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi wakati huu wa vuguvugu la vyama vya siasa vya upinzani.
Katika hatua nyingine, Mnec huyo amesema CCM ngazi zote katika manispaa ya Singida,zianze sasa kujipanga vema kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Wakati huo huo,Mazala aliongoza kwa ufanisi mkubwa harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la ofisi ya CCM tawi la Mwaja ambapo Jumla ya shilingi 855,500 zimechangwa.
Kati ya kiasi hicho, shilingi 325,500 ni fedha taslimu na zilizosalia ni ahadihuku Mazala binafsi amechangia shilingi laki tatu taslimu.
Aidha,mwenyekiti wa CCM kata ya Mitunduruni na mfanyabiashara maarufu mjini Singida,Velarian Kimambo,alichangia mifuko ya saruji 10.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...