Jumamosi, 15 Juni 2013

ARUSHA KAMPENI ZA UCHAGUZI ZAENDELEA KUPAMBA MOTO

Naibu katibu mkuu akijadiliana jambo na mmoja wa wazee wa CCM kata ya kaloleni jioni hii kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa udiwani Jijini Arusha
Kada wa chama cha mapinduzi(CCM) mtela mwampamba akizungumza na wanachama  wa CCM na wananchi wa kata ya kaloleni jijini Arusha.Katika moja ya sentensi zake Mtela Mwampamba amewaomba wana kaloleni kumchagua mgombea wa CCM siku ya jumapili.Pia amesisitiza vijana kuachana na siasa za kutumika,siasa za kupoteza muda,Siasa za maandamano.Amehoji ni kwanini mikutano ya CHADEMA lazima mtu afe au vurugu zitokee?hivyo dawa moja ya kuachana na siasa za vurugu ni kuichagua CCM.
Wanakaloleni muulizeni Mbunge wa Arusha,Lema kama anajua maana ya maendeleo yaliyopo na serikali ya CCM.Muulizeni Lema tokaanze kazi ya ubunge amewaletea maendeleo gani hapa Arusha,anapoteza muda na rasilimali kupambana na Meya wa halmashauri.Huo ni upuuzi.

Mamia ya wananchi wa Kaloleni wakisikiliza sera za CCM muda huu viwanja vya kaloleni
CCM HOYEEEEEE

Aliyekuwa mmoja wa wanachama wa CHADEMA waliomsaidia Lema kupata Ubunge Ndugu Mboya akimnadi mgombea wa CCM Ndugu Emmmanuel Thobias

Wanachi wamejitokeza kwa wingi sana kwenye hii kata ya kaloleni kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa udiwani..

"Tutashindaaaa,Mchagueni diwani wa CCM kwa maendeleo ya kaloleni"

Kushoto ni mgombea wa Udiwani kata ya kaloleni akiwa na Aliyekuwa diwani wa CHADEMA  Bi.Rehema Mohamed ambaye sasa ni kada wa chama cha mapinduzi

Naibu katibu mkuu wa CCM Tanzania Bara,Mh:mwigulu Nchemba akihutubia mamia ya wanachama wa CCM na W ananchi wa kata ya kaloleni.Naibu katibu mkuu amewaomba wana kaloleni kuachana kabisa na kufikiria kuhusu mgombea wa Upinzani kuwaletea maendeleo,kwa sababu mgombea yeyote wa upinzani hana ilani wala sera ya kuleta maendeleo.Ni mgombea pekee wa CCM ndiye ilani yake na sera zake zinafanyiwa kazi na serikali.Hivyo naomba mchague

Mkutano unaendelea na Naibu Katibu mkuu wa CCM akihutubia mamia ya wananchi wa kata ya kaloleni jioni hii tar.14/06/2013

Naibu katibu mkuu Mh:Mwigulu Nchemba"CCM ni moja,Sisi ni wamoja na hatutenganishwi na mtu.naomba mjitokeze kupiga kura siku ya jumapili.CCM tunaamini katika amani na utulivu tena demokrasia ndio msingi wetu.Hivyo lazima tujitokeze kupiga kura na tumpe ushindi mgombea wa CCM kuhakikisha maendeleo yanafika hapa kaloleni

"Hao wapinzani wamewafanyia nini?Wanatumia zaidi ya milioni 200 kuzindua kampeni kwa helkopta,mwisho wa mikutano yao wanakinga bakuri kuomba miamia zenu"

Viva CCM Viva .hapa wananchi wakimshangilia Naibu katibu Mkuu Mh:Mwigulu Nchemba kwa hotuba yake nzuri na yenye kuleta mwamko wa maendeleo kwa wananchi wa kata ya kaloleni

Mchagueni Emmanuel Thobias kwa maendeleo ya kata ya kaloleni.

Nasisitiza,hakuna mtu wa kuwatishia kwenda kupiga kura,Nendeni kwenye vituo vya kupigia kura mkiwa na shada za kupigia kura,naomba bendera na mavazi ya kichama muachane nayo siku ya uchaguzi.Vurugu hazitakuwepo,ulinzi umeimalishwa".

"Njia pekee ya kuwashinda kwa kishindano hawa wapinzani ni sanduku la kura,hakikisha unapiga kura na unakuwa balozi wa kuwahimiza watu wengine wakapige kura"Mh:Mwigulu Nchemba

Naibu katibu mkuu akiwasikiliza wananchi wa kata ya kaloleni waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa udiwani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...