Jumapili, 9 Juni 2013

CCM DAR WAKUTANA NA UJUMBE WA VIETNAM LEO


Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida,
akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti
cha Vietnam, Hoang Binh Quan, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam, leo
Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, nape Nnauye aliyesimamia
mazungumzo hayo. (Picha na Bashir Nkoromo)
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (aliyesimama) akifunga mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramdahani Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Viatnam, kwenye Ofisi za CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo.

 Mjumbe wa Chama Cha bKimomunisti cha China, akimpa zawadi Madabiba baada ya mazungumzo yao.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine.
Na Pius Ntiga, UHURU FM
Chama Cha Kikomunisti Cha Vietnam-CVP, kimekitaka Chama Cha Mapinduzi-CCM, kutoogopa kuwafukuza uanachama wake wasio na nidhamu ambao hawazingatii maadili na kanuni za Chama kilichpo Madarakani.
          Pia Chama hicho cha CVP kimesisitiza kuwa ni bora kuwa na wanachama wachache kuliko kuwa na wanachama wengi wasio na nidhamu.
          Kauli hiyo ya Chama cha Kikomunisti Cha Vietnam, imetolewa leop Juni, 8, 2013 na Kiongozi wa Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho Bwana HOANG BINH QUAN wakati wa mazungumzo na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Mkoa wa Dar es salaam ambao umeongozwa na Mwenyekiti wake Ramadhan Madabida.
          Katika mazungumzo hayo, Bwana QUAN pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa Chama cha siasa kudumisha nidhamu ndani ya Chama na kuachana kabisa na kasumba ya kuwa na wanachama wengi huku miongoni mwao wakiwa ni wasaliti wakubwa ndani ya Chama.
          Kwa sababu hiyo Bwana QUAN akakiomba Chama Cha Mapinduzi ambapo katika mazungumzo yao yalihuidhuliwa pia na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE kutowaonea haya wanachama wasaliti ndani ya Chama.
          Hata hivyo Chama Cha Mapinduzi-CCM kupitia kwa Katibu wake Mkuu ABDULRAHMAN KINANA, tayari kilishatoa kauli kama hiyo ya kuwa ni bora kuwa na wanchama wachache wenye nidhamu kiliko kuwa na wanachama wengi wasio na nidhamu.
          Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida ameuambia ujumbe wa Chama hicho cha Kikomunisti Cha Vietnam kuwa CCM itaendelea kudumisha uhusiano wa siku nyingi na Chama hicho huku akisistiza umuhimu wa wananchi wa Vietnam kuja kuwekeza nchini hasa katika Mkoa wa Dar es salaam kutokana na fursa mbalimbali zilizopo.
          Pia pamoja na mambo mengine amezungumzia haja ya vyama hivyo viwili vya CCM pamoja na CVP kubadilishana wanachama kwa kwenda kujifunza namna mbalimbali za Kiuongozi ndani ya vyama hivyo.
          Madabida ameainisha maeneo machache ya uwekezaji katika jiji la Dar es salaam kuwa ni pamoja na eneo la uvuvi kupitia Bahari ya Hindi, kilimo pamoja na  sekta ya umeme hivyo akaomba wawekezaji kutoka Vietnam kuja kuwekeza Tanzania.
          Akishukuru kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi kuhusiana na ugeni huo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE amesema ujio wa viongozi hao umefungua ukuraa mpya wa ushirikaino katika Nyanja mbalimbali za kisiasa hasa ikizingatiwa historia ya muda mrefu kati ya CCM na CVP.
          Katika kusisitiza umuhimu wa ushirikiano huo Nape amesema CCM daima itaendelea kushirikiana na Chama cha CVP kutokana na misingi iliyoachawa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere pamoja na Rais wa Kwanza wa Vietnam HO CHI MIHN.
          Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Afisa wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa CCM Makao Makuu Bi.Juliana Chitinka, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ernest Charle, Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Silvester Mrope pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Salum Madenge.
          Ujumbe huo wa Chama Cha Kikomunisti Cha Vietnam-CVP, umemaliza ziara yake ya kichama hapa nchini na ulitarajiwa kuondoka kurejea nchini kwao Vietnam leo mchana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...