Jumapili, 9 Juni 2013

WAZIRI MKUU ATEMBELEA JUMUIYA YA SACOMA, LONDON NCHINI UINGEREZA

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Mizengo Pinda, akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Sacoma group, Bwana. Sam Ochieng, namna ambavyo bidhaa za Matunda na Mboga mboga kutoka nchini Kenya zinavyopakiwa, kusafirishwa na hatimaye kuuzwa kwenye soko la Spitfield nchini Uingereza, kwa kupitia Jumuiya ya Sacoma. Umoja huo wa Sacoma wenye lengo la kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wa africa ya Mashariki. Mheshimiwa Waziri Mkuu, alifanya ziara kwenye Soko la Spitafields, lililopo Stratford nchini Uingereza, kwa lengo la kujionea shughuli za Jumuiya ya Sacoma inavyoendesha shughuli zake kwenye soko hilo na jinsi ambavyo Jumuiya hiyo imeweza kuwasaidia Wakulima wa Matunda na Mboga kutoka nchini Kenya, kupata soko la kuuza Bidhaa zao hapa nchini Uingereza.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, akiangalia na kupata maelezo ya Ubora wa bidhaa unaotakiwa kupata soko nchini Uingereza. Pichani, mstari wa pili, (kwanza kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Ungereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, kwanza (kulia) ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, Uingereza Bwana Yusuf Kashangwa, maofisa wa Ubalozi na Viongozi kutoka Tanzania ambao wameambatana na Waziri Mkuu nchini Uingereza kwenye Mkutano unaofanyika leo ambao unahusu jinsi ya kutokomeza njaa na umuhimu wa Lishe bora kwa Mama na Watoto Duniani (Hunger and Nutrition). Mkutano huo ambao umeandaliwa na Asasi za kiserikali na zisizo za Kiserikali, unakutanisha nchi kubwa Duniani, zijulikanazo kama G8, Wadhamini, Wachangiaji na Watoa misaada kwenye Asasi hizo, zenye lengo la kutokomeza njaa duniani na kusaidia kuwapatia Wamama na Watoto Lishe bora. NA MATUKIO MICHUZI BLOG
Mheshimiwa Waziri Mkuu, akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Soko la Spitalfields. Kushoto ni Meneja wa Masoko wa Kikundi cha Sacoma, Mama Perez Ochieng - Meneja wa Masoko wa Jumuiya ya Sacoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Peter Mizengo Pinda, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, kilichopo London, Bwana Yusuf Kashangwa, wakiangalia bidhaa mbalimbali kutoka nchini Kenya na kupeana ushari jinsi gani ambavyo wanaweza kuwasaidia Wakulima na Wafanyabiashara wa Tanzania kwa kupitia Jumuiya ya Sacoma, kuweza kuuza Bidhaa zao nchini Uingereza.
Mheshimiwa waziri Mkuu akisikiliza maelezo kutoka kwa Dada Perez Ochieng - CEO na Bwana Sam Ochieng wa Sacoma, jinsi ya Bidhaa za Maua kutoka nchi za Afrika ya Masharikina zinavyoweza kuingizwa na kuuzwa hapa Uingereza.
Waziri Mkuu wa Tanzania,Mheshimiwa Peter Mizengo Pinda , akitoa maoni yake jinsi Serikali za nchi za Afrika ya Mashariki zinavyoweza kushirikiana kuwasaidia Wakulima kuweza kupata nafasi za kuuza Mazao yao nchini Uingereza. Pichani vile vile Viongozi wa Soko la Spitfield, Sacoma na Ujumbe kutoka Tanzania, ambao unaongozana na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwenye Mkutano wa kutokomeza njaa na umuhimu wa Lishe Bora kwa Mama na Watoto. Mkutano huo ambao umeandaliwa na Asasi binafsi na za Kiserikali, unawakutanisha Serikali kubwa Duniani (G8), Wadhamini na Watoa Misaada kwenye Asasi hizo zenye lengo la kutatua tatizo la njaa na Lishe Bora Duniani.
Pichani, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda, Balozi wa Tanzania, Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe (kulia), dada Perez Oohing, Meneja wa Soko la Spitalfields na Viongozi wengine wa Jumuiya ya Sacoma nchini Uingereza.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Balozi, wakiwa kwenye picha ya Pamoja na Viongozi na Wahusika na Wawakirishi wa Jumuiya ya Sacoma.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda, akijibu na kumsikiliza Mwandishi wa Tanzania kwenye Magazeti ya Citizen, Bwana Fredy Macha, mara baada ya kumalizika ziara ya kutembelea Soko la Spitalfields lililopo Stratford nchini Uingereza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...