Jumatatu, 17 Juni 2013

DIWANI MPYA KATA YA MIANZINI

 Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana ameibuka mshindi wa uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mianzini uliofanyika jana kwa kupata kura 1283, huku Mgombea wa Cuf akipata kura 494, Chadema wakiambulia kura 315 na ADC walipata kura 26, NRA kura 9 na Mgombea wa NCCR Mageuzi akiambulia kura 1. Bawji amemzidi mshindi wa pili kwa zaidi ya nusu ya kura.
 Mara baada ya matokeo kutangazwa na tume kupitia kwa Afisa Mtendaji wa Kata, Wanachama wa CCM waliletewa matokeo yale na kusomwa na Mkurugenzi wa uchaguzi wao ambaye ni Katibu kata wa Mianzini wa CCM, Abdallah Kihuku mbele ya hadhara ya Wana CCM waliofurika katika ofisi za kata . Picha na Emmanuel Shilatu wa http//: www.ndgshilatu.blogspot.com
 Mshindi mteule wa Udiwani wa Kata ya Mianzini, Athman Bawji Mbwana akiongea machache kwa Wana CCM mara baada ya kutawazwa kuwa mshindi. Bawji anaziba nafasi iliyokuwa wazi kufuatia kifo cha diwani wa kata hiyo.
 Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, Ramadhan Madabida akiwashukuru wana CCM kwa umoja na mapambano ya dhati yaliyopelekea ushindi wa CCM. Huu ndio uchaguzi wake wa kwanza tangu awe Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam na ni uchaguzi mdogo wa pekee wa udiwani kwa Mkoa wa  Dar Es salaam.


 Katibu wa Mkoa wa CCM, Abdillah Mihewa naye pia akitoa yake ya moyoni.
 Katibu wa Wilaya ya Temeke wa CCM, Ndg Robert Kihaka akiwashukuru Wana CCM kwa uvumilivu wao na jitihada zao zilizozaa matunda mema.

Mida ya jioni, tayari wana CCM walishaanza heke heka za kushangilia ushindi.
 
Mawakala  wa CCM wakiwasili katika ofisi za kata kwa kuwasilisha taarifa za matokeo ya uchaguzi kwa chama

 Mjumbe wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Emmanuel John akiwasili toka kuwakusanya mawakala wa CCm kwenye vituo vyao vya kupigia kura.


 Wana CCM walifurika katika ofisi za kata ya Mianzini wakishangilia ushindi. Ilikuwa ni raha tupu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...