Jumatatu, 17 Juni 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, AFUNGA TAMASHA LA ASILI LA WATU WA MANGAPWANI UNGUJA JANA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi wakati akiwasili kwenye viwanja vya Mangapwani jana Juni 15, 2013 kwa ajili ya kufunga rasmi Tamasha hilo lililoanza Juni 14.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya akina mama wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika Tamasha la Asili la Watu wa Mangapwani, alipofika kufunga rsmo tamasha hilo jana Juni 15, 2013, mjini Munguja.
 Katika Tamasha hilo kulikuwa na mashindano ya michezo mbalimbali ya asili, kama Bao la Kete, Kufua Nazi, na kama mchezo huu pichani vijana wakishindana kukwea Minazi, ambapo kwa upande wa michezo Tamasha hilo lilihitimishwa kwa mchezo wa fainali ya Soka.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mlezi wa Tamasha la asili la Watu wa Mangapwani, Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Mwinyi Jamari Ramadhan Nasib, pamoja na baadhi ya viongozi, kwa pamoja wakifurahia mchezo wa kukwea minazi wakati wa Tamasha hilo. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPO CHINI

 Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kufua Nazi, wakichuana kufua Nazi hizo ambapo kila mmoja alitengewa jumla ya Nazi 20, na mchezaji wa kwanza (kushoto) ndiye aliibuka mshindi kwa kuwaacha wenzake na Nazi nyingi zaidi wakiendelea kuchuana wawili. 
 Mshindi akiinua juu Nanga yake ya kufulia Nazi kuashiria kumaliza kabla ya wenzake na kuibuka mshindi.
 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa na michezo ya asili cha Luperwa Zanzibar Group, chenye maskani yake Bububu, wakitoa burudani wakati wa hafla ya kufunga Tamasha hilo, lililofungwa na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunga mlango wa Kibanda cha Makuti kama ishala ya kufunga rasmi Tamasha hilo la Watu wa Mangapwani, jana Juni 15, 2013, lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Juni 14. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...