Alhamisi, 18 Julai 2013

MAKAMU WA RAIS DK.BILAL KUFUNGUA KONGAMANO LA UWEZEZAJI IJUMAA

IMG_7600MNA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MAKAMU wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la Uwekezaji katika mkoa wa Tabora litakalofanyika keshokutwa (Ijumaa) kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam.
 
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dares Salaam na Mkuu wa Wilaya wa Tabora Mjini Suleiman Kumchaya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa  Tabora Fatuma Mwasa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano hilo.
 
“Tunamkaribisha mtu yeyote aje kuwekeza Tabora kwa kuwa soko tayari lipo. Tunataka kupandisha hadhi ya mkoa wa Tabora ili hali ya umasikini iondoke,” alisema Kumchaya.
 
 Akizungumzia kuhusu hali ya mkoa huo, Kaimu Katibu Tawala wa  Mkoa wa Tabora, Longino Kazimoto alisema    ni mkubwa kuliko miko mingine hivyo wanataka uwe na maendeleo makubwa ndio maana wanawakaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.
   
Kazimoto  aliongeza kuwa mkoa huo una rasilimali za kutosha , ambazo ni misitu hekari 75,685 sawa  na asilimia 44, ambapo asali inapatikana kwa wingi, mifugo ipatayo milioni 3.2, matunda, hivyo  wawekezaji wanaweza kuanzisha viwanda vya kusindika.
 
 Aidha alisema mkoa huo hivi sasa kwa mwaka unaingizia Serikali Pato la Taifa   Sh. bilioni 1.2 na pato la mwananchi  wa kawaida ni  Sh. 560,783 kwa mwaka.
 
Kazimoto alisema  katika mkoa huo kuna vikundi 46 vya vijana ambavyo vimeandaliwa ili kuweza kufuga nyuki kwa kisasa ili kuweza kupata asali ya kusafirisha nje ya nchi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...