Alhamisi, 26 Septemba 2013

ABDULRAHMAN KINANA AWAWEKA SAWA WANA MUSOMA, AWAAMBIA WAHOJI MAENDELEO YAO

2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amepanda kwenye kivuko cha MV Musoma kinachovusha watu kutoka Wilaya ya Rorya na Musoma kikitokea Kinesi leo akielekea Musoma mjini tayari kwa kumalizia ziara yake mkoani Mara, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, Kinana amemaliza ziara yake ya mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara leo kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape N nauye.Ndugu Kinana amesema ni haki ya wananchi kuhoji maendeleo yao kwani wanasiasa wa vyama mbalimbali vikiwemo vya upinzani vilipita na kutoa ahadi tena wengine waliahidi kutoa asali na maziwa huku wengine wakiahidi wananchi kuwa wakiwachagua watajenga barabara za marumaru.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MUSOMA MARA3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika kivuko hicho pamoja na wananchi, kushoto aliyembeba mtoto ni Katibu Mkuu wa UWT Taifa Amina Makilagi4Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akiwa amesimama katika ukingo wa kivuko hicho pamoja na wananchi.5Msafara wa magari ukitoka kwenye kivuko cha MV Musoma mara baada ya kuwasili mjini Musoma leo ukitokea wilayani Rorya.6Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  wa tatu kutoka kulia naKatibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye wa pili kulia  wakishuka kwenye kivuko cha MV Musoma mara baada ya msafara wake kuwasili mjini Musoma leo7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye  wakiwapungia mkiono wananchi waliojitokeza kuwapokea mjini Musoma8Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vikundi mbalimbali vya sanaa mjini Musoma9Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Jailos Chilewa Mhandisi mkazi  wa mradi mkubwa wa maji wa ziwa Victoria  uliopo Bukanga Makongo nje kidogo ya Manispaa  ya Musoma wakati alipokuwa akikagua ujenzi wa mradi huo leo.10Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Jailos Chilewa Mhandisi mkazi  wa mradi mkubwa wa maji wa ziwa Victoria  uliopo Bukanga Makongo nje kidogo ya Manispaa  ya Musoma wakati  akitoa maelezo ya mradi huo,  kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Bw. Christopher Sanya11Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na ukaguzi wa mradi huo.12Ukaguzi ukiendelea13Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Samson Winani wakati akikagua mradi wa hospitali ya mkoa ya Rufaa Kwanga mjini Musoma, ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kuanza kuendelea hivi karibuni.14Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi ya CCM Kata ya Bweri mjini Musoma.15Hii ndiyo ofisi yenyewe.16Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akipokea zawadi jogoo kutoka kwamwenyekiti wa shina namba 6 mama ThabithaAmina Idd mara baada ya kutembelea shina hilo na kuongea na wanachama.17Katibu Mkuu wa Umoja wa wanawake UWT Mama Amina Makilagi akiwahutubia wana Musoma leo kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma leo.18Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akizungumza na wanaMusoma leo kwenye viwanja vya Mukendo.19Hawa ni miongozi mwa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo.20Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Musoma leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...