CHAMA cha
Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro kimeagiza kata ya Kibaoni kuitisha mkutano mkuu wa halamashauri kuu ya kata ya
Kibaoni iliopo wilayani Kilombero ili kumjadili katibu kata wa CCM wa kata hiyo
kwa tuhuma za ulevi.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Morogoro Innocent Kalogiries Alitoa agizo hilo jana wakati
akizungumza katika mkutano mkuu wa halimashauri ya kata hiyo.
Alisema
alilazimika kutoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wajumbe wa
Halmashauri kuu ya kata hiyo kuwa katibu wa kata hiyo John Uwaya alikuwa amekithiri kwa vitendo vya ulevi na
hivyo kushindwa kutimiza majukumu yake ya kazi.
‘’ Hili lipo
ndani ya uwezo wenu, itisheni mkutano wa halmashauri kuu ambao ndio
uliomchagua, muende na ajenda ya kumsimamisha kisha kumwondoa . Alisema.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa imefika wakati kwa sasa viongozi wasiofaa ni vema wakaenguliwa
kama wenyewe hawataki kujiengua ili kunusuru chama.
Hata hivyo
mwenyekiti huyo aliwataka viongozi wa wanachama wa CCM kuwa hakuna chama
madhubuti kama CCM na kwamba wasijaribu kushawishika na vyama vingine kwani
amani na utulivu wan chi utatoweka.
‘’
Mtakaoumia ni nyie na watoto wetu, hao mnaowaona wanahangaika na vyama vya
upinzani ikitokea kuvunjika amani wanauwezo wa kukimbilia nchi nyingine’’
Alisema.
Alisema kuwa
yapo mataifa ambayo yalijaribu kubadilisha chama kwa lengo la kudhani watapata
manufa na badala yake wakaambulia vita.
Kwa upande
wao wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kata ya Kibaoni waliomba CCM wilaya hiyo
kutowaingilia na kubeba wagombea wao wa udiwani katika uchaguzi mdogo na badala
yake wawaachie wachague mtu ambaye wao wanaona anawafaa.
‘’ wilaya
tunaomba ituachie kata katika uchaguzi huu wenyewe, wapo viongozi ambao tayari
wameanza kuja’’ alisema Said Tomas Lupia.
Kata ya
kibaoni ipo katika mchakato wa kutafuta diwani baada ya diwani wa kata hiyo
Salumu Msika kufariki dunia mapema mwezi juni mwaka huu
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni