MKUU wa wilaya ya Kilombero Hasani Masala amelalamikiwa kwa
kitendo cha kuvunja uongozi katika serikali za vitongoji vitatu katika kijiji cha Mkangawalo kata Mngeta
wilaya Kilombero mkoani Morogoro na kusimika viongozi wengine.
Malalamiko hayo yametolewa jana na wananchi wa kata hiyo ya Mngeta wakati wa
ziara ya katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM mkoa wa Morogoro wilayani Kilombero.
Wananchi hao walisema kuwa mkuu wa wilaya huyo alivunja
serikali hizo Mei 23, 2013 baada ya
kufika kijijini hapo na kudai kuwa viongozi wa serikali hizo wanatuhumiwa kwa
ubadhirifu wa fedha na kwamba wanatakiwa kusimamaishwa ili uchunguzi ufanyike.
Mkuu huyo wa wilaya alipofika kijijini hapo alivunja
serikali za vitongoji vya Itongoa A, Itongoa B na Mgudeni kwa madai kuwa
viongozi wake wanatuhumiwa kwa ubadhilifu wa
fedha.
Mmoja wa wanachi hao Richard Mwamwanga alisema mkuu wa wilaya huyo alipofika kijijini hapo
alivunja uongozi huo kwa madai kuwa uchunguzi hauwezi kufanyika wakati viongozi
hao wakiwa madarakani na aliahidi kupeleka mrejeho wa uchunguzi huo.
‘’ Chakushangaza ni kwamba baada ya wiki moja, Mei 30, 2013
uchaguzi ulifanyika na hadi sasa miezi sita imepita DC huyu hajaleta mrejesho
wowote’’ Alisema.
Hata hivyo alisema kuwa awali wananchi hao walipomuuliza
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero Hazimina Mbilinyi alidai kuwa
utaratibu uliofanywa na mkuu huyo wa wilaya sio sahihi na kwamba atachukua hatua.
‘’Baada ya muda mkurugenzi huyo alifika
tena na kuwasimika viongozi hao jambo ambalo liliwachanganya wananchi hao’’
Alisema Mwamwanga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya
ya Kilombero David Ligazio alisema kuwa baada ya kutokea tatizo hilo alimwagiza mkurugenzi wa
halmashauri hiyo kumshauri mkuu wa wilaya hiyo juu ya sheria husika za Tamisemi
kwa kuwa uongozi huo umechaguliwa kisheria na kwamba vinatakiwa kuvunjwa
kisheria.
Alisema kuwa yeye kama msimamizi
mkuu wa halamshauri hiyo hatambui uongozi huo uliowekwa na mkuu wa wilaya
kinyume na taratibu na kwamba amewaagiza
mkurugenzi kufika katika kijiji hicho na kutoa tamko hilo la halmashauri.
Alisema kuwa kutokana na mgogoro
huo hadi sasa halmashauri hiyo imesitisha kutoa posho kwa viongozi hao wa pande
hizo mbili hadi sheria itakapofuata mkondo wake.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya huyo Hasan Masala alikiri kusimamisha kwa
serikali hiyo kutokana na tuhuma mbalimbali zilizokuwa zikiwakabiri
viongozi hao na kusema kuwa kama uchaguzi ulifanyika yeye hajui.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni