MWENYEKITI
wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro Inocent Kalogeris ameagiza kutohamishwa watendaji katika ngazi mbalimbali hadi
mikutano mikuu na halimashauri za CCM
katika ngazi husika zikae na kusomewa mapato na matumizi.
Mwenyekiti
huyo alisema hayo jana wakati akizungumza katika kikao cha halimashauri kuu ya
CCM kata ya Kibaoni wilayani Kilombero mkoani hapa.
Alisema
kuwa mtendaji yeyote asiruhusiwe
kuondoaka katika eneo lake la kazi bila kusoma mapato na matumizi na kujua kama
hakuna ubadhilifu wa aina yeyote.
‘’ Sio kwa
watendaji tu bali hata viongozi wa kuchaguliwa, hakuna kujiuzuru hadi wanachama wajue mapato yao’’ Alisema.
Alisema kuwa
kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watendaji wasio waadilifu kufanya ubadhilifu
sehemu moja na kuhamishiwa sehemu nyingine jambo ambalo alisema linaendelea
kukiumiza chama cha Mapinduzi.
Aidha
aliwataka viongozi kila mmoja kutimiza wajibu wake katika eneo lake badala ya
kutegemea viongozi wa ngazi za juu kuwatatulia matatizo yao.
Hata hivyo
alisema kuwa kwa sasa umefika wakati wa kuweka viongozi wenye maadili ambao
wanaweza kukiongoza chama na sio kuchagua viongozi wanaotoa rushwa.
‘’ Tusipoikataa rushwa chama tunakiua,
tunapotea ndugu zangu, fedha unayopewa inakuhukumu kwa kipindi chote cha
uongozi uliomchagua’’ Alisema.
Mwenyekiti
huyo alisema kuwa CCM mkoa wa Morogoro kamwe hautavumilia kuona viongozi
wanaogombea na kwamba watakaobainika kuwa na hila kama hiyo na kwamba watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na
kuwaengua katika nafasi zao.
mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni