Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi CCM kupitia kundi la
vijana Jonas Nkya akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa
habari mjini Morogoro juu ya kauli za katibu wa chipukizi na hamasa
Taifa Paul Makonda za kusema waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa hafai
kuwa kiongozi, wala mwenyekiti wa CCM taifa na hata pia kuwa amirijeshi
mkuu akimtuhumu kuwa fisadi ambapo MNEC huyo amejia juu kusema kuwa
amekurupuka na kauli na kwamba sio msemaji wa UVCCM wanamshangaa.
Kama maisha ya Mjini yamemshinda aje vijijini tumpe shamba alime sio
kuuza maneno ili apete fedha za kuishi, Lowasa alikuwa kiongozi kabla ya
Makonda kuzaliwa, amekurupuka kuaongea kitu asichokijua na wala hana
ridhaa ya kusema hayo,atolewe UVCCM atatuvuruga, Ni MNEC mwingine wa
UVCCM Ramadhani Kimwaga akiongea na waandishi wa habari mjini Morogoro.
JUMUIYA ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM
mkoa wa Morogoro Imemtaka katibu wa
chipukizi na hamasa Taifa Paul Makonda kuaomba radhi waziri mkuu mstaafu Edward
Lowasa , wazee, vijana na viongozi wa dini
kwa kauli aliotoa za uchochezi
na za kukigawa chama.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wajumbe wa
halmashauri kuu ya CCM NEC kupitia kundi
la vijana Jonas
Nkya na Ramadhani Kimwaga walisema kuwa kauli hizo si za UVCCM ni za Makonda binafsi.
Nkya alisema kuwa vijana wa mkoa wa Morogoro
wamehuzunishwa na matamshi ya Makonda aliotoa juzi wakati alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kumshutumu Lowasa kuwa hafai
kuwa kiongozi wan chi hii, wala kuwa amrijeshi mkuu sambamba na mwenyekiti wa
CCM Taifa.
‘’ UVCCM hatupo kwaajili ya kutengeneza Marais, na
si jukumu letu, na wakati wake haujafika hivyo tunamshangaa Makonda kuanza
kuzungumzia masuala ya Urasi na
kuwachanganua nani anafaa na nani hafai
wakati sio kazi yake na aingii katika kikao chochote cha maamuzi ya kumteua
mgombea Urais’’ Alisema.
Alisema kuwa hakuna kikao chochote cha baraza
kilichokaa na kutoa tamko kama hilo na kwamba utaratibu wa UVCCM na CCM kwa
ujumla maamuzi yote hutoka katika vikao halali.
‘’Sisi UVCCM hatutaki kuingiza masuala binafsi
na jumuiya yetu ambayo yatapelekea
kukigawa chama na jumuiya zake, hivyo vijana lazima tubadirike’’ Alisema
Aliwataka viongozi wa dini, vijana mbalimbali
aliowatamka pamoja na Lowasa kupuuzia
kauli hiyo na kwamba UVCCM wako pamoja
viongozi wa dini, vijana mbambali na hata waziri mkuu mstaafu.
Kwa upande wake Kimwaga alisema kuwa kauli ya
makonda ya kusema kuwa lowasa hafai kuwa kiongozi ni kukitukana chama kwa
kumteua kugombea ubunge jimbo la Monduli na pia kumteua kugombea ujumbe wa NEC
nafasi ambazo ni nyeti katika chama.
‘’ Lowasa amekuwa kiongozi wa muda mrefu katika CCM
hata kabla makonda hajazaliwa na hadi sasa, hivyo kauli za Makonda zinaonyesha
ni mtu mwenye kuweweseka na hastaili
kuwa kiongozi, hivyo hakuna budi kuenguliwa katika nafasi hiyo kutokana na
kushindwa kuitumikia’’ Alisema
Alisema kuwa kuendelea kuwepo katika nafasi hiyo
makonda kutasababisha kugawa UVCCM pamoja na kukivuruga chama .
‘’ Mtu ukimtuhumu kuwa fisadi mla rushwa ni lazima
uwe na ushahidi na kama anao basi aende kushitaki mahakamani sambamba na katika
vyombo husika kama takukuru, na kama hajui aje tumwelekeze ofisi zao zilipo’’
Alisema
Alimshauri makonda kuja vijijini ili wamtafutie shamba la kulima kuliko kukaa mjini kwaajili ya kuuza
maneno ili apate fedha za kumwezesha kuishi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni