Yaani siwezi kuwa mpumbavu kuwaruhusu eti mkatandike mikeka katika
kiwanda cha Mtibwa mkidai fedha zenu, Ni mkuu wa wilaya ya Mvomero
Antoni Mtaka wakati akiongea na wafanyakazi, wastaafu, na wakulima wa
kiwanda cha sukari cha Mtibwa wilayani humo ambao walitaka kujua muafaka
wa madai yao.
Ni lazima tujadiliane kwa makini tupate ufumbuzi, anayesema maneno
yangu ni siasa, siasa haziko hapa ziko huko. Ni Dc Mtaka akiwajibu
wakulima hao waliomwambia kuwa anayoongea ni siasa na kwamba hakuna
utekelezaji.
Tunachotaka hapa leo ni kulipwa fedha zetu na sio vinginavyo, ni mmoja
wa wakulima wa miwa Mtibwa Turiani akiongea katika mkutano huo wa
maelfu ya watu.
Tufanye hivi leo ni Jumanne, hawa watu tuanze kuwalipa ifikapo Alhamisi
au unasemaje? meneja msaidizi Kiula akinong'ona na meneja mkuu wa
kiwanda hicho Hamad Yahaya.
KIWANDA cha sukari cha Mtibwa kilichopo wilaya ya Mvomero
kimetakiwa kusitisha shughuli zake za uzalishaji hadi watakapomaliza kulipa
madeni ya wakulima miwa na wafanyakazi
wa kiwanda hicho.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Mvomero antoni
Mtaka baada ya mabishano ya muda mrefu juu ya madai ya wakulima wanayodai
kiwanda hicho zaidi ya bilioni 1.9 za mauzo ya miwa na mishahara ya wafanyakazi
wa kiwanda hicho.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa shughuli za huduma ya afya
zinazotolewa na kiwanda hicho pamoja na
ulinzi na shughuli za uhasibu zitaendelea ili kuwezesha wananchi hao kupata
mafao hayo mwishoni mwa wiki hii kama ilivyoahidiwa na uongozi wa kiwanda
hicho.
Aidha kutokana na mabishano na kutoelewana katika mkutano
huo kamati ya ulinzi na usalama na baadhi ya viongozi wa serikali na
halimashauri na wawakilishi wa wanasiasa
walilazimika kukaa chemba kwa muda wa nusu saa kwaajili ya kujadili suala hilo
na kuja na maamuzi hayo na kusitisha shughuli hizo.
Hata hivyo mkuu huyo alisema kuwa kutokana na malalamiko ya
wakulima na wafanyakazi hao ya kuwa watoto wao wamasimamsihswa shule
kutokana na kukosa ada ameagiza
wanafunzi hao wote kuendelea na masomo hadi hapo wazazi wao watakapolipwa fedha
zao.
Awali Uongozi wa kiwanda hicho ukiwakilishwa na meneja mkuu
Hamad Yahaya Juma alisema kuwa kiwanda hicho kinatarajia
kuanza kulipa madeni hayo kuanzia Januari 30 mwaka huu.
Meneja huyo alisema kuwa kiwanda hicho kilikwama kulipa
madeni hayo kutokana na uingizwaji
mwingi wa sukari hapa nchini na hivyo kusababisha sukari ya kiwanda hicho
kushindwa kupata soko.
Pia alisema kuwa makubaliano ya mwisho baina ya uongozi wa
kiwanda hicho na wakulima na wafanyakazi hao ni kuwalipa ifikapo Februari 25
mwaka huu na kwamba alidai wadai hao
walikiuka na kuanza kudai kwa stahili nyingine ambayo anadai inaushawishi wa
kisiasa.
Kwa upande wa wafanyakazi wa kiwanda hicho ambao walikuwa
wakidai kiwanda hicho milioni 190 aliahidi kulipa Februari 15 mwaka huu.
Baada ya mkuu wa wilaya kutoa maazimio hayo wananchi hao
ambao walikuwa na jazba walishusha jaziba zao na kutawanyika taratibu katika
eneo hilo ambalo awali ililazimikwa kuwekewe ulinzi mkubwa wa askari wa
kutuliza fujo wakiwa na bendara na mitutu ya bunduki kuhakikisha usalama
unapatikana katika eneo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni