Richard Haule akiwa na mwenzake ambaye badae alitoweka wakisukuma mkokoteni huo.
Hilo ni eneo la nyuma la uwanja wa jamuhuri linalopaka na uwanja wa golf likiwa limegeuzwa dampoo.
Baadhi ya wanafunzi waliokutwa wanasoma katika eneo hilo la uwanja wa Jamuhuri jirani kabisa na dampoo hilo huku harufu mbaya na moshi vikitanda katika eneo hilo.
Habari zaidi Soma hapo chini.
CHAMA cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro kimeitaka halmashauri ya Manispaa ya Morogoro kuacha kugeuza eneo la uwanja wa Jamuhuri kama sehemu ya Dampoo la kutupia takataka.
Katibu wa CCM
mkoa wa Morogoro Rojas Romuli alisema hayo jana wakati akiongea na waandishi wa
habari ofisini kwake juu ya hali halisi ya uwanja huo unaomiliki na CCM.
Alisema
Halmashauri hiyo kupitia vikundi vyake vya uzoaji wa taka vimekuwa vikitupa
takataka wanazozoa katika mitaa mbalimbali ya
Kata ya Boma na kuzitupa hapo hali inayohatarisha maisha ya watu
sambamba na kuharibu mandarin ya uwanja huo.
‘’ Tumeshawapa
taarifa ili wazoe takataka zote walizomwaga katika eneo la uwanja huo
tunasubiri utekelezaji, hii ni mara ya pili sasa awali walishawahi kufanya
hivyo wakazoa naona sasa wanarudia tena’’ Alisema.
Alisema uwanja
huo ambao unategemewa kwa shughuli mbalimbali za mkoa na kitaifa unatakiwa
kuwekwa katika mazingira safi na salama na sio kugeuzwa kama dampoo.
Hata hivyo katibu huyo alisema wanatarajia
kuboresha mazingira yote yanayozunguka
uwanja huo kwa kukata miti iliozidi ovyo .
Alisema sambamba
na hilo pia wanatarajia kufanya ukarabati katika jingo hilo maeneo ya nje ya
uwanja kwa kupiga plasta na kupaka rangi ili uweze kuvutia zaidi.
‘’ Tunataka
uwanja wa Jamuhuri uwe kivutio cha watu kuja kupumzika na kuvuta hewa safi,
tunataka kupanda miti ya maua na matunda na kuweka bustani nzuri za maua’’
Alisema.
Hata hivyo katibu
huyo alisema wanamshukuru mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro Paskari
Kihanga kwa kuwasaidia kupata kisima katika uwanja huo ambacho kitasaidia kuwa
na maji ya uhakika.
Mmoja
wa wanakikundi wanaozoa takataka katika kata ya Boma alidai kuwa yeye
alipewa maelekezo ya kumwaga takataka hapo na bosi wake aliyemtaja kwa
jina moja la Mama Sanga.
Richard
alisema kwa muda mrefu sasa wamekuwa wakimwaga takataka hapo na badae
kulipia manispaa kwaajili ya kuzizoa na kwamba anaona ni utaratibu
sahihi.
''
Kwanza mimi nasngaa sijui nani kaamua kuzichoma hizi takataka hapa,
maana baada ya kujaa huwa tunalipia manispaa alafu wanakuja kuzichoma''
alisema.
Baadhi
ya wanafunzi wanaosoma katika eneo jirani na dampoo hiyo walidai
wanapata adha kubwa kutokana na harufu mbaya na kwamba wanaomba serikali
kuchukua hatua ili kuepuka magonjwa ya milipuko yanayoweza kuwapata.
''
wanazidi kuzijaza mwisho zitafika hadi eneo la hosteli yetu pale,
maisha yetu yapo hatarini alisema mmoja wa wanafunzi ambaye hakutaka
jina lake litajwe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni