Nasra
akiwa na mama anayemlea kwa sasa Josephin Joel kutoka kambi ya ya wazee
ya Fungafunga iliopo mjini hapa, akiwa katika chumba cha ICU hospitali
ya rufaa ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu baada ya kufichwa
katika box kwa miaka 4 na mama yake mkubwa Mariam Said baada ya mama
yake mzazi kufariki mwaka 2010.
Hali
ya Narsa kwa sasa imezidi kutengemaa ,kunawili na kuonekana kama mtoto
mwenye nuru kama anavyoonekana tofauti na alivyookolewa kutoka katika
box siku tano zilizopita hapo mama huyo mlezi akimpatia chakula iana ya
wali na samaki anaopendelea Nasra.
Hapo Nasra akiwa ameshika kikombe kwa mikono yake mwenyewe ilioonekana awali kutokuwa na nguvu baada ya kuomba maji ya kunywa Petter Mwita Mtetezi wa haki za watoto mkoa wa Morogoro akiwa na Nasra katika kitanda anacholala mtoto huyo kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro. alishukuru vyombo vya habari kwa kutoa habari zilizofanya Nasra kupatiwa misaada mbalimbali.
Habasi zaidi Soma hapo Chini.
Hapo Nasra akiwa ameshika kikombe kwa mikono yake mwenyewe ilioonekana awali kutokuwa na nguvu baada ya kuomba maji ya kunywa Petter Mwita Mtetezi wa haki za watoto mkoa wa Morogoro akiwa na Nasra katika kitanda anacholala mtoto huyo kwenye wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro. alishukuru vyombo vya habari kwa kutoa habari zilizofanya Nasra kupatiwa misaada mbalimbali.
Habasi zaidi Soma hapo Chini.
SAKATA la Mtoto aliyeishi
katika box kwa miaka 4 sasa limechukua sura mpya baada ya nyumbani kwa
mama mkubwa wake Mariam Said kukutwa kuna shimo kubwa lililojaa
maji hali inayozidi kuwachanganya wakazi wa mjini hapa.
Wakiongea
na mwandishi wa habari hizi mwenyekiti wa mtaa wa Azimio anakoishi
mama huyo , Tatu Mgagala alisema Mei 22 polisi walifika mtaani hapo wakiwa na
mtuhumiwa huyo na kukuta mlango umefungwa na kuamua kuvunja
ili waweze kuingia ndani kuangalia mazingira ya nyumba hiyo.
Alisema
baada ya kuingia ndani ya chumba cha Mariam walikuta kuna giza nene kutokana na
chumba hicho kuzibwa na mabox na hivyo kutoa mabox hayo .
Alisema
baada ya kutoa mabox hayo waliona shimo kubwa lenye maji karibu na eneo
lilipo box alikokuwa akiishi mtoto huyo na alipoulizwa mama huyo
kulikoni na kuacha maji ndani huku akijua kuna ugonjwa wa Dengue
alidai maji hayo huyatumia kunawa miguu na mikono usiku kabla ya kulala.
‘’ Ndani
ya nyumba hiyo sehemu zote zimesakafiwa isipokuwa eneo hilo ambalo lilichimbwa
shimo hilo’’ alisema. Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo
imebainika kuwa mariamu na mumewe kwa muda mrefu walikuwa hawajaoga na hivyo
kulazimishwa kuoga wakiwa mbaroni .
Kwa upande
wake mtetezi wa haki za watoto Petter Mwita alisema
watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mei 26 mwaka huu ni Mariam ,mumewe
Mtonga Omari na baba mzazi wa mtoto huyo Rashid Mvungi.
Alisema
ndani ya nyumba ya mama huyo zikukutwa picha ambazo zinaonyesha kuwa mtoto huyo
alikzaliwa akiwa hana ulemavu na kwamba inadaiwa ulemavu huo alipata kutokana
na ukatili alikofanyiwa na walezi hao
‘’ Vitendo
walivyofanya wote hawa watatu ni vya kikatili na vinatakiwa kupigwa kwa nguvu
zote nah ii itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii.
Alisema
baadhi ya mitandao ya kijamii ilivumisha kuwa mtoto huyo alinyanyasika na mama
yake mkubwa huyo kwa madai kuwa mama yake mzazi alikufa na ugonjwa wa
Ukimwi ambapo alisema suala hilo kwa mtoto huyo halipo kwani tayari
alishafanyiwa kipimo hicho na kubaini hana ugonjwa huo.
Hata hivyo
alisema kwa sasa wamemtafuta mama mlezi wa Mtoto huyo kwaajili ya kumuhudumia
katika huduma zote na anlipwa kwa kazi hiyo.
Naye
Josephina Joel mama ambaye kwa sasa ndiye anamlea mtoto huyo alidai yeye amechukuliwa
kutoka katika kambi ya kulelea wazee Fungafunga ya mjini hapa na kwamba anajua
uchungu wa watoto hivyo kwake anaona hakuna changamoto zozote anazopata kwa
mtoto huyo.
‘’ Mimi
niliachwa na mume wangu naishi Fungafunga nalelewa na Ustawi wa jamii kwangu
kumlea mtoto huyo nachukulia kama mjukuu wangu na nafurahia na sioni shida
yeyote’’ Alisema.
Aidha
alisema mtoto huyo hupendela kula chipsi mayai, wali nyama au samaki pamoja na
juice huku akionyesha kukataa ugali wala maziwa.
Mtoto huyo
kama kitu hataki anafumba macho, kwa mfano ukimwambia nikupe ugali anakataa, au
maziwa , lakini pia hapendi kuoga na ukimwambia kuoga au kula vyakula
asivyotaka anakwambia badae’’ Alisema
Mwandishi wa
habari hizi alifanikiwa kufika nyumbani kwa Mvungi Kihonda eneo la Maduka
kumi anakoishi na mkewe wa ndoa kwa lengo la kutaka kujua jinsi huyo
mke alivyochukulia jambo hilo na kuwafukuza waandishi wa habari kwa madai
ya kuwa wakaandike wanavyojua wao.
‘’ Ehe
waandishi wa habari mnataka nini tena kwangu uwiiii, mimi sijui chochote,
ondokeni, huku akiondoka kueleka sebuleni waliko mgeni wake
aliyemtmbulisha kama wifi yake huku akimwambia kwa lugha ambayo ilisikika kwa
neno lililoashiria wandishi wa habari hao’’ Alisema
Hata
hivyo waandishi wa habari walifika nyumbani hapo nao wakiwa
nyuma yake wakarudi naye hadi eneo alipo wifi yake na kujaribu kudadisi
zaidi jambo bila mafanikio zaidi ya kutawala kimya kwa muda wa dadki kumi
na ndipo alipoohoji tena kuwa wanataka nini.
Hata hivyo
mama huyo ambaye anaonekana ni mjamzito alionekana kupandisha pumzi na kushusha
hali iliosababisha kushindwa kuongea na hivyo waandishi hao kuamua kuondoka
kurejea mjini.
Kamanda wa
polisi mkoani hapa alithibitisha kukamatwa kwa baba wa Nasra Said na
kwamba yuko nje kwa dhamana na aatafikishwa mahakamani pamoja na watuhumiwa
wezake Mei 26 mwaka huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni