Ijumaa, 11 Julai 2014

DAKTARI FEKI ATIWA MBARONI, AKAMATWA HOSPITALI YA MKOA WA MOROGORO

Huyo ndiye Karume kauzu Habibu, daktari feki aliyekamatwa  katika hospitali ya mkoa wa Morogoro akitibu wagonjwa, amekuwa akivaa koti leupe mithiri ya  Daktari. kwa sasa anashikiliwa na polisi.

Amekutwa na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kinaonyesha anarudia mtihani katika kituo kimoja mjini Morogoro, ni mkazi wa Kigoma, kwa sasa alikuwa akiishi Liti manispaa ya Morogoro.
Polisi wanafanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...