Jumapili, 14 Septemba 2014

MZINGA YAJENGA KITUO CHA UTAFITI NA ULENGAJI SILAHA,

 Waziri wa ulinzi Dk Husein Mwinyi akiangalia samani zinazotengenezwa na shirika la Mzinga la mkoani Morogoro kwaajili ya matumizi ya shule, ofisi na nyumbani wakati wa kilele cha sherehe za miaka 40 ya shirika hilo.
 Dk Husen Mwinyi akimpatia cheti cha kutambua mchango wake mmoja wa wafanyakazi waanzilishi wa shirika hilo.
 Kikundi cha burudani cha shirika la mzinga  wakiwa katika sherehe hizo baada ya kutumbuiza.
 Wafanyakazi na familia za wanajumuiya ya shirika la Mzinga wakiwa katika viwanja vya sherehe hizo juzi.
 Waziri Mwinyi akisalimiana na mkuu wa majeshi  Devis Mwamunyange baada ya kuwasili katika bwalo la jeshi la Magadu manispaa ya Morogoro.
 Dk Mwinyi akiweka jiwe la msingi katika eneo la Magadu linapojengwa jengo la kituo cha utafiti na ulengaji wa silaha.
 Waziri huyo akipata maelezo ya  jinsi mashine ya kutengeneza matofali ya njanja  iliotengenezwa na shirika hilo.
 Mkuu wa majeshi Mwamunyange,  na waziri Mwinyi wakibadilishana mawazo katika kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya shirika la Mzinga, kulia ni meneja wa shirika hilo Meja Jenerali  Dk Charles Muzanila.
 Mkuu wa majeshi Mwamunyange akipata maelezo ya ujenzi wa nyumba  maalum za kulala wageni zinazojengwa katika eneo la  Bwalo Magadu  sambamba na bwawa la kuogelea la kimataifa ujenzi utakaogharimu kiasi cha sh milioni 700
habari zaidi.

WAZIRI wa ulinzi Dk Husein Mwinyi, ameliagiza shirika la Mzinga la Mkoani Morogoro kuhakikisha wanatengeneze zana zote za kijeshi ili kupunguza gharama kwa Serikali kuziagiza nje ya nchi.

Waziri huyo alisema hayo jana katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 40 kwa shirika hilo.
‘’ Shirika hili lilipoanzishwa mwaka 1970 lilikuwa kwaajili ya kuzalisha mazao ya kijeshi,   sasa imefikia wakati kwa shirika hili kutengeneza zana zote hata zile ambazo kwa sasa tunaagiza nje’’ alisema.
Hata hivyo Dk Mwinyi alilitaka shirika hilo la Mzinga katika mango wake mkakati wa mwaka 2011 -2026 kuhakikisha wanazalisha bidhaa bora zaidi ili kuweza kuziuza katika taasisi za serikali, mashirika na  watu binafsi.
Alisema kwa kufanya hivyo kutasaidia kujiongezea kipato na kupunguzia Serikali mzigo wa ruzuku kwa shirika hilo.
Awali meneja wa shirika hilo Charles Muzanila alisema wameanza ujenzi wa kituo cha utafiti na mafunzo ya kulenga shabaha ili kuwezesha vyombo vya usalama na raia wanaomiliki silaha kuweza kupatiwa mafunzo hayo.
‘’ Kwa sheria ijayo kila mtu ambaye anataka kumiliki silaha ni lazima apate mafunzo ya jinsi ya kutumia silaha hilo kwa usalama, na kila mwaka ni lazima ahakikiwe kabla ya kupewa kibali cha silaha hiyo ili kuona kama anaweza kumiliki au laa’’ alisema dk  Muzanila.
Muzanila alisema ujenzi huo utagharimu kiasi cha sh bilioni 11 za Tanzania, ambapo unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi sita kuanzia sasa.
Alisema ujenzi huo utahusisha jengo la karakana, darasa, maabara na stoo ya kuhifazia zana za kijeshi, pamoja na uwanja wa kufanyia mazoezi hayo ya kulenga shabaha.
Muhandisi mshauri wa shirika hilo  Donald mwakatonga alisema  kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuchukua watu 20 kwa wakati mmoja na kwamba mafunzo hayo yataendeshwa kwa mfumo wa komputa.
‘’ Kila komputa mmoja itakuwa inatunza kumbukumbu za mtu mmoja kuona kama amelenga shabaha ngapi’’ Alisema.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo mkuu wa majeshi  Devis Mwamunyange,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...