Jumamosi, 6 Septemba 2014

VIKUNDI VYA WAJASIRIMALI MORO WAFANY A SHEREHE YA KUMPONGEZA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI

 Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akipokelewa na Viongozi wa Vikundi vya wajasiriamali  Kutoka  Manispaa ya Morogoro Mara baada ya kuwasili tayari kushirikiana nao katiaka sherehe iliyoandaliwa na vikundi hivyo kwajili ya kumpongeza Mbunge huyu kwa msaada wake anaotoa na kuwawezesha katika shuguli zao za ujasiriamali.
 Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood  Akisalimiana na wanachama wa vikundi Mbalimbali kutoka kwenye kata mbalimbali manispaa ya Morogoro.




 Wanachama wa vikundi vya wajasiriamali manispaa ya morogoro wakimsikiliza kwa makini Mlezi wa Vikundi hivyo ambaye pia Ni Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjin Mh Aziz Abood.




 Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akitoa hotuba yake wakati wa shere ya kupongezwa iliyoandaliwa na vikundi vya wajasiriamali kutoka manispaa ya Morogor.Ambapo Mbunge huyo amesema ameshatekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa kuomba kuchauliwa kuwa mbunge na kilichobaki anamalizia kwa muda huu uliobakia kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.Akielezea kwa kifupi alisema Barabara Nyingi za manispaa ya Morogoro kwa saa zimejengwa kwa kiwango cha lami.Amekarabati vituo vya afya katika kata mbalimabila,Amelipia ada wanafunzi wasio na uwezo zaidi 7OO ,Pia amedhibiti matumizi mabaya ya fedha za wananchi.

Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akitoa hotuba yake wakati wa shere ya kupongezwa iliyoandaliwa na vikundi vya wajasiriamali kutoka manispaa ya Morogor.Ambapo Mbunge huyo amewahakikikshia wanachama wa vikundi hiyo kuwa nao bega kwa bega katika shuguli zao za kila siku.na muda wowowte wakiitaji msaada toka kwake wasisite kwenda kumwona.Ambapo wanachama wa vikundi hiyo wamempongeza mbunge huyo kwa mssa wake mkubwa wa kuviwezesha vikundi hiyo na wamemuahidi kuwa Mbuinge wao na mwaka kesho watamchukulia fomu ya ubunge ili aendelee kuwa mbunge wao maana hawajona mbunge kama yeye.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...