Alhamisi, 6 Juni 2013

HOTUBA YA KAIMU AFISA MTENDAJI MKUU WA TTCL BW. JOTHAM LUJARA KATIKAMAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI

.
………………………………………………………………….
Kwa niaba ya Afisa Mtendaji wa TTCL, viongozi na wafanyakazi
wenzangu wa TTCL, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwako Mkurugenzi
mkuu na wafanyakazi wa Muhimbili u kwa kukubali ombi letu la kuja kufanya usafi
katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kama mjuavyo, Siku ya mazingira duniani kilele chake huadhimishwa kitaifa kila mwaka
tarehe 5 Juni. Maadhimisho haya kimataifa yatafanyika Brazil. Kauli Mbiu ya
maadhimisho ya mwaka huu Kimataifa ni FIKIRI, KULA: HIFADHI MAZINGIRA (Think – Eat –
Save).
Kitaifa ujumbe unaoongoza madhimisho haya ni “Fikiri kabla ya Kula: Hifadhi
Mazingira”.
TTCL imeshiriki katika wiki ya Mazingira kwa kufanya usafi hapa katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili leo tarehe 5 Juni 2013 .
Kama Kauli mbiu yetu inavyosema TTCL – Huleta watu karibu, ndio maana tumeamua
kushiriki katika siku hii hapa Muhimbili ili kutoa hamasa kwa watu na jamii kwa ujumla
kuona umuhimu wa kutunza mazingira katika sehemu wanazoishi na sehemu
zinazowazunguka.
Pia tutakuwa tumeionyesha jamii kuwa kampuni yetu haipo tu kuhudumia wateja, bali
kuhudumia jamii na wahitaji kwa ujumla.
MATIBABU MTANDAO NA TTCL
Page 2
TTCL kwa kushirikiana na baadhi ya hospitali nchini wameannza kutoa huduma
ya matibabu mtandao (Tele Medicine) kwa kutumia mkongo wa taifa wa
mawasiliano, hivyo kupunguza gharama za kufuata usumatibabu nchi za nje
kama India, Uingereza, Ujerumani na Afrika Kusini. Hospitali za KCMC na
Bugando zimeunganishwa na TTCL na zimeshaanza kutoa huduma ya
matibabu mtandao kupitia huduma ya fibre ya TTCL ambayo ni teknolojia ya
mawasiliano ya kisasa yenye ubora na viwango vya juu. TTCL kwa kushirikiana
na Muhimbili na Amana wanaweza wakaanza kutoa huduma za matibabu
mtandao kama wanavyofanya hospitali ya KCMC.
MATATIZO
Huduma hizi za matibabu mtandao ambazo ni mkombozi wa wanyonge
zinakwamishwa na waru wanaoujumu miundombinu ya TTCL kwa kukata nyaya
zinazopitisha mawasiliano pamoja na kukata Mkongo wa taifa wa mawasiliano.
WITO
Tunatoa wito kwa wananchi na jamii kwa ujumla kuwa na mazoea ya kufanya
usafi katika sehemu wanazoishi na sehemu zinazowazunguka, kuepuka kutupa
taka ovyo na kuhakikisha wanatupa taka kwenye vyombo husika . TTCL
tunaashimisha siku hii kwa kuongozwa ka kauli mbiu yetu ya’TTCL- huleta watu
karibu ‘kwa kufanya usafi katika hospitali hii inayotibu wananchi wengi, sababu
ni tunajali wananchi ambao ndio wateja wetu. Hivyo tunatimiza kauli mbiu hiyo
kwa kuwa karibu na wananchi kibiashara na kazi za kujitolea.
Tunapoashimisha siku hii y a mazingira duniani, tunaiomba jamii na wananchi
kwa ujumla watusaidie kufichua uhalifu dhidi ya nyaya za TTCL na mkongo wa
Taifa wa Mawasiliano kituo cha polisi kilicho karibu au ofisi zozote za TTCL zilizo
karibu nawe. Lengo ni kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na
huduma ya matibabu mtandao, elimu mtandao, biashara mtandao , utalii
mtandao n.k.
TTCL – HULETA WATU KARIBU

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...