Jumatano, 5 Juni 2013

SERIKALI KUZICHUKULIA HATUA KALI HALMASHAURI ZISIZOTEKELEZA MIRADI YA MAJI

Kauli hiyo imetolewa mapema leo na waziri mkuu,Mizengo Pinda alipokuwa akifungua mkutano wa mwaka wa kujadili utekelezaji wa miradi ya maji vijijini unaofanyoka kwa siku tano jijini Arusha,ambapo zaidi ya
washiriki 500 kutoka sekta mbalimbali za  maji wamehudhulia.
Waziri Pinda alisema kuwa serikali haitasita kuchukua  hatua kali kwa wahandisi wa maji wa wilaya ambao hadi kufikia muda huo watakuwa hawajakamilisha  ujenzi wa miradi yote kwani hadi sasa halmashauri
zote zimeshapokea fedha zinazotesheleza ujenzi wa miradi yote mitano.
Hata hivyo alisema kwa kipindi cha miaka mitatu 2013-2016 serikali katika sekretarieti ya maji mapango huo unalenga kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kwenye maeneo ya vijijini ,huku akisema hali hiyo ni kutokana na asilimia kubwa ya wananchi waishio vijijini  hawapati huduma ya maji ipasavyo kutokana na miradi mingi kuchakaa bila kukamilika kutokana na usiomamizi duni wa watendaji.
Awali akimkaribisha waziri mkuu, waziri wa maji Prof Jumanne Maghembe alisema katika mwaka 2013-2014 serikali imepanga kutekeleza miradi 1000 ya ujenzi wa  maji  mjini na vijijini utakao wanafaisha watu laki
8.7 kwa nchi nzima.
Aidha alisema  utekelezaji wa mpango huo unalenga kutekeleza mpango wa milennia ifikapo 2020 ili kuwanufaisha wananchi walio wengi hususani waishio vijijini  na kuwafikia kwa asilimia  62 ifikapo mwaka 2014.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...