Ijumaa, 15 Novemba 2013

TATIZO LA BEI YA KOROSHO KUPATIWA TIBA YA KUDUMU

1a (2)Sultan Linyama Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kata ya Nakapanya Wilayani Tunduru Mkoa wa Ruvuma  jana mara baada ya kuwasili katika kata hiyo akitokea Wilayani Masasi Mkoani Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku 23 kwenye  mikoa ya Ruvuma. Mbeya na Njombe akikagua miradi mbalimbali na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM na kuhamasisha wananchi katika suala zima la kushiriki katika shughuli za maendeleo, Tatizo kubwa la mikoa ya Kusini hasa Mtwara, Lindi na Ruvuma ni kuhusu bei ya zao la korosho ambapo Katibu Mkuu Kinana amesisitiza kuwa Chama cha Mapinduzi kitahakikisha suala hilo linashughulikiwa kwa umakini na Serikali ikishirikiana na taasisi zinazohusika na zao hilo ili kukomboa uchumi wa wananchi wa eneo hilo hasa kwa kuhakikisha viwanda vya kubangua korosho vinajengwa na vile ambavyo vilibinafsishwa na havifanyi kazi kunaandaliwa utaratibu ambao utawafanya waekezaji wengine kupewa ili vifanye kazi na kutatua tatizo la bei ndogo ya zao hilo inayolipwa na wanunuzi wa korosho zisizobanguliwa,Katika ziara hiyo  Kinana ameongoza na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi na Dr. AshaRose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamtaifa (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-TUNDURU)9Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisimikwa usultani na mzee wa kimila Alli Hassan Omar Linyama mara baada ya kuwasili katika kata ya Nakapanya Wilayani Tunduru jana.11Wananchi wakicheza ngoma wakati walipokuwa wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana10Mzee wa kimila Alli Hassan Omar Linyama kushoto akijiandaa kufanya kazi yake kabla ya kumsimika Ndugu Abdulrahman Kinana kuwa Sultan Linyama5Dk. AshaRose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akizungumza na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma mama Verena Shumbusho.3Wananchi wakiwa wamefurika kwa wingi katika mkutano wa hadhara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akihutubia mkutano wa hadhara jana.8Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akielekeza jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani akizungumza na wananchi katika kata ya Namiungo wilayani Tunduru.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...