HALMASHAURI
ya manispaa ya Morogoro imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni
50 kwa wafanyabaishara walikokuwa wakiendesha biashara zao bila leseni.
Afisa
habari wa manispaa hiyo Liliani Henerico alisema hayo jana wakati akitoa
taarifa ya oparesheni ilioendeshwa na mansiapaa hiyo katika nyumba za
kulala wageni na maduka mjini hapa.
Alisema
oparesheni hiyo ilifanywa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Aprili mwaka
huu na kwamba jumla ya biashara 54 zilifugiwa kutokana na kushindwa kulipa
faini hizo.
Alisema
katika zoezi hilo faini za leseni zilikuwa ni shilingi 4,540,000 ambapo
mapato ya ada za leseni yalikuwa ni 45,786859 n hivyo kufanya jumla ya
makusanyo hayo kuwa ni shilingi milioni 50,326,859.
Aidha
afisa habari huyo alisema zoezi hilo linaendelea kuhakikisha wafanyabiashara
wote wanafata taratibu na kuepuka kukwepa kodi.
Kwa upande
mwingine afisa habari huyo alisema manispaa hiyo ilianza zoezi la kukagua
nyumba katika manipaa hiyo kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.
Alisema
utekelezaji wa zoezi hilo la usafi wa mazingira hadi sehemu za makazi ya
wananchi ni agizo la mkuu wa mkoa la kutaka halmashauri zote kuhakikisha
zinakuwa safi ili mkoa wa Morogoro uweze kupata tunzo ya usafi kitaifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni