WANAFUNZI
wa vyuo
vikuu wametakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwaajili ya kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu
masomo yao badala ya kutumia kwa kujifurahisha kama ambavyo wengi wamekuwa
wakifanya hivyo.
Hayo yalisemwa jana na naibu makamu wa mkuu wa chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Josephat
Itika wakati wa kongamano la wanafunzi
wanaosoma masomo ya uhasibu chuoni hapo.
Alisema
mara nyingi wanafunzi hao wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kwa kujiburudisha na
kwamba mitandao hiyo ingekuwa na manufaa
kwao kama wangetumia kupata vitu vinavyowasaidia katika masomo yao.
“
Katika mitandao kuna fulsa nyingi za elimu, watumie fulsa hizo kuendeleza fani
zao, wapunguze muda wa kuchati na meseji za kujifurahisha tu’’ Alisema.
Hata
hivyo alisema katika kongamano hilo wanafunzi walipata fulsa
ya kukutana na wataalamu mbalimbali wa
masuala yanayohusu uhasibu na kuweza kubadilisha uzoefu kwa lengo la kwenda na
wakati.
Aidha
alisema moja ya changamoto inayowakabili wasomi ni soko la ajira ambalo
hubadilika kila siku hivyo ni lazima kuhakikisha wanakidhi mahitaji hayo.
‘’
Sisi kama waadhiri tunachofanya ni kufanya utafiti kila wakati na kujua nini
kinahitajika katika soko la ajira na ndipo tunakuja kuwaletea wanafunzi wetu,
sio kukazania kusoma vitabu tuu’’ Alisema.
Naye
Hawa Tundui muhadhiri katika chuo hicho alisema kwa sasa wahitimu ni wengi
hivyo soko la ajira ni gumu
ukilinganisha na miaka ya 1980 hivyo ni lazima kwa vyuo huria vikaangaia jinsi
gani ya kuwafundisha wanafunzi wao kulingana na soko la ajira.
Alisema
kongamano hilo linawabadilisha mtazamo wanafunzi hao kujua mbinu mbadala za
kuweza kujiajiri badala ya kubakia na mtazamo wa kupata ajira.
Husen
Maneno mwanafunzi wa mwaka wa pili
anayechukua masomo ya biashara katika chuo hicho alidai kumekuwa na
ucheleweshaji wa kubadili mitala kwenda na wakati hapa nchini na kwamba hiyo ni changamoto kubwa
inayowakabili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni