. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina
Kombani amewataka wakulima kusahau yaliopita juu ya vyama vya ushirika
na kuvifufua kwani ndio mkombozi wao, Alisema hayo wakati wa kuhitimisha
kilele cha siku ya wakulima 88 mkoani Morogoro.
Kombani akisindikizwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiq,
pamoja na mwenyekiti wa TASO kanda ya Mashariki Mohamed Mzee ,a katibu
wake Rafael kumtunza mwana dada huyo aliyekuwa kivutio cha burudani
katika maonyesho hayo baada ya kupiga danadana kwa zaidi ya nusu saa
bila mpira kumponyoka.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Antoni Mtaka akiwa katika moja ya bada
linalozalisha mahindi ya lishe lijulikanoalo kama CPP Tanzania Co.LTD,
Mtaka ni miongoni mwa wakulima wa mbegu hiyo mkoani Morogoro, baadhi ya
wananchi walimwambia Mtaka kwamba ameonyesha kipaji chake kuwa ni
kilimo na kumtaka kuwashawishi viongozi wengine kuiga mfano wake,
'' Mimi ni mkulima, nimeanza kuonyesha kipaji changu, sio kusubiri hadi
ustaafu ndio unaanza kutafuta cha kufanya,'' alisema Mtaka.
Mahindi yaliotumika kuonyesha mfano katika banda hilo yanatoka katika
shamba la Mkuu huyo wa wilaya ya Mvomero Mtaka ambayo amelima wilayani
humo.
Viongozi wa wilaya ya Kilombero wakiwa katika maonyesho hayo siku ya kilele cha 88 mkoani Morogoro.
Maafande wa JKT kanda ya mashariki wakipokea zawadi ya ushindi wa kampuni za zana za kilimo ambapo wamenyakua nafasi ya kwanza.
Makamo mkuu wa chuo kikuu cha kilimo SUA Profesa Monella akipokea
zawadi baada ya kushika nafasi ya kwanza katika kilimo na utafiti.
Meya wa Manispaa ya Morogoro akiwa katika maonyesho hayo na viongozi wengine mkoani hapa.
Msanii kutoka wilaya ya Bagamoyo akionyesha fani yake kwa kuigiza
kujikata panga ambalo lilionekana kuingia mwilini pasipo kutokwa na
damu.
Wasanii kutoka Mtibwa wakionyesha burudani ya sarakasi kwa kutumia viti vulivyopangwa juu ya chupa za bia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni