Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul, akionyesha moja ya silaha zilizowahi kutumika katika matukio ya uharifu hivi karibuni.
habari zaidi soma hapo chini.
WATU watano wanashikiliwa na polisi mkoani hapa, kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya ujambazi mkoani Morogoro na Dodoma, akiwemo mwanamke mmoja.
Kamanda wa
Polisi mkoani hapa Leonard Paul, alisema watu hao walikamatwa Septemba 17
mwaka huu majira ya mchana huko Kijiji cha Luhembe tafara ya Mikumi wilayani Kilosa.
Alisema
majambazi hayo yanadaiwa kufanya tukio
la ujambazi mkoani Dodoma kisha kukimbilia mkoani Morogoro,ambapo polisi wa
mikoa hiyo miwili ndio walifanikisha kukamatwa kwao.
Alisema mmoja wa majambazi hao alikamatwa mkoani
Dodoma,baada ya kufanya uharifu na kwamba ndiye alifanikisha kukamatwa kwa
wenzake baada ya msako mkali wa polisi.
Hata hivyo
kamanda huyo alisema baada ya kuwakamata majambazi hao ,walifanikiwa kukamata
bunduki aina ya MSG yenye namba za usajili 380859.
Alisema mbali
na bunduki hiyo polisi hao walifanikiwa kukamata meno ya tembo mawili aliokutwa
nayo mmoja wa majambazi hao huko Luhembe.
Hata
hivyo
kamanda huyo alisema polisi wa mikoa hiyo miwili wanaendelea kutafuta
silaha na majambazi wengine , waliohusika na tukio hilo na kuwataka
wananchi kutoa taarifa za watu
wanaowatalia mashaka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni