Jumanne, 21 Januari 2014

MANISPAA YA MORO YATOA MILIONI 600 UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA .

 Meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akipata maelezo kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule ya ujirani iliopo kata ya Kihonda Philemon Kibuja wakati wa ziara ya kamati ya fedha ya manispaa hiyo.
 Tumeleta milioni 10 kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika shule hii, ili wanafunzi wetu waweze kusoma vizuri. Amiri Nondo akiongea katika ziara hiyo.


 Wanafunzi wa shule ya msingi Ujirani wakiwa katika moja ya chumba cha madarsa katika shule hiyo.
 Tumeleta milioni 600 katika Hospitali ya wilaya inayojengwa hapa Kiegea ili kurahisisha huduma ya afya kwa wakazi wa huku na jirani. meya wa manispaa ya Morogoro Amiri Nondo akitoa taarifa kwa kamati hiyo.

 Meya huyo akiangalia moja ya nguzo inayojengwa katika Hospitali hiyo ya wilaya ya manispaa ya Morogoro.
 Madiwani na watendaji wa manispaa ya Morogoro wakiongea na injinia wa kampuni ya Mzinga inayofanya ujenzi katika hospitali hiyo ya wilaya.
 Kwa kawaida ujenzi wa kampuni ya mzinga tunaukubali, ni maneno ya Maya Nondo.
 Baadhi ya wagonjwa waliofika kupata huduma katika kituo cha afya cha Uhuru maarufu kama Nunge .
 Diwani wa kata ya Kingo Fidelis tailo akimpa maelezo meya wa manispaa ya Morogoro kuwa hospitali hiyo imeelemewa, . hakuna stoo, madaktari wanatumia chumba kimoja wanne, huduma za usiri kwa wagonjwa hakuna.
 Nimechelewa kidogo maana ratiba sikuipata vizuri, karibuni jamani Mjimpya, ni diwani wa Mjimpya Wensilaus akiwakaribisha madiwani wenzake waliotembelea stendi mpya ya magari yanayokwenda nje ya manispaa ya Morogoro.
Hapa ndio yatapakia magari ya Mgeta, stendi hii itapunguza msongamano pale mjini .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...