Mwenyekiti wa umoja wa Vijana Taifa Sadifa Juma Khamis akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chipukizi uliofanyika katika shule ya sekondari ya wasichana ya Kilakala mjini Morogoro.
Mlezi wa chipukizi Taifa Dk Abdala Kigoda Akitoa neno la shukrani baada ya mkutano kufunguliwa.
Baadhi wa wagombea wa Chipukizi wakisubiri hatma yao.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chipukizi Taifa wakifutilia mkutano huo kwa makini.
Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Sictus Mapunda akiteta jambo na Mlezi wa chipukizi Dk Abdalla Kigoda Nje aya ukumbi mara baada ya mkutano kufunguliwa..
HABARI ZAIDI , SOMA HAPA.
MWENYEKTI wa Umoja wa Vijana Taifa Sadifa Juma Khamis
amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kwa malezi ya kuilea jumuiya hiyo na kazi kubwa ya kuleta maendeleo ya taifa.
Sadifa alisema hayo jana wakati akifungua mkutano mkuu wa
Chipukizi Taifa uliofanyika katika shule ya sekondari ya Kilakala mjini
Morogoro.
Alisema kuwa chama cha Mapinduzi lina jukumu kubwa la kulea
jumuiya zake na kwamba chimbuko la viongozi wazuri linatokana na Chipukizi.
Aliwataka wazazi na walezi kuwalea chipukizi katika maadili
mema ili waweze kuwa viongozi bora wanaoandaliwa kwaajili ya miaka ya badae.
Akitolea mfano alisema kuwa viongozi wengi walioko
madarakani kwa sasa walipita katika tanuru la chipukizi na Uvccm na kwamba
walilelewa katika maadaili mazuri ambayo yamefikisha kuwa viongozi waadilifu.
‘’ Rais Kikwete ni miongoni mwa mjumbe wa baraza la umoja wa
vijana waanzilishi na kwamba leo tunamwona ndio kinara wa nchi’’ Alisema
Kwa upande wake mlezi wa Chipukizi taifa Dk Abdala Kigoda
aliwataka baada ya uchaguzi huo kumalizika makundi yavunje kwani yanadhoofisha
chama.
Hata hivyo alisema kuwa umoja na mshikamano ndio
utakaosababisha CCM kushika hatamu milele na kwamba kamwe hawataki kusikia CCM
ikiitwa chama cha Upinzani kwani ndio chama pekee kilichopatia uhuru wan chi ya
Tanzania.
Naye katibu mkuu wa UVCCM Taifa Sixtus Mapunda alisema kuwa
alipokea hoja mbalimbali kutoka kwa makatibu wa hamasa na chipukizi ikiwemo ya
kutaka kushiriki mkutano mkuu wa CCM taifa kama wanavyoshiriki makatibu wa
Jumuiya hiyo.
Alisema hoja nyingine ni kutaka ajira za kudumu kwa makatibu
hao kama walivyo makatibu wa jumuiya jambo ambalo alisema madai yote
wamayapokea na kwamba watayafanyia kazi.
Mwisho
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni